Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WADAU wa Usimamizi wa kemikali taka kutoka sekta ya mafuta na gesi kutoka taasisi za umma na binafsi wamehimizwa kuendelea kusimamia sheria,kanuni na sera kuhakikisha hakuna madhara yatakayotokana na matumizi ya kemikali.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Magdalena Mtenga wakati akifungua warsha ya Usimamizi wa Kemikali taka katika sekta ya gesi na mafuta iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi za umma na binafsi.

Mtenga aliyemuwakilisha Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Ester Makwahiya ,amesema ipo haja ya kukumbusha wadau umuhimu wa kuwa na matumizi sahihi ya kemikali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa kati unaokwenda sambamba na ujenzi wa uchumi wa viwanda.Amesema matumizi ya kemikali hayaepukiki na hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia na kwamba kemikamil inatumika katika matumizi mbalimbali yakiwamo ya viwandani na majumbani.

Amesema hivyo ipo haja ya kuwa na matumizi sahihi ya kemikali kwani iwapo hakutakuwa na matumizi sahihi kuna hatari ya kupatikana kwa madhara kwa mtumiaji."Kuna mifano ya athari ambazo zinatokana na matumizi mabaya ya kemikali na miongoni mwa athari hizo ni kupatwa kwa ulemavu wa viungo," amesema.Amesema katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama Serikali imechukia hatua mbalimbali za kuhakikisha kemikali inatumika katika matumizi sahihi na salama kwa kufuata sheria,kanuni,Sera na miongozo iliyopo.


Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bi. Magdalena Mtenga, akifungua (kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira)) warsha ya wadau wa Usimamizi wa Kemikali na Kemikali Taka za Sekta ya Mafuta na Gesi inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, Dar es Salaam .

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na washiriki wa warsha kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa ufunguzi 
Mtaalam wa Jiolojia kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Bw. Simon Nkenyeli (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na masuala ya usimamizi wa petroli kwa washiriki wa warsha ya Usimamizi na Usimamizi wa Kemikali taka za sekta ya Mafuta na Gesi inaeyoendelea jijini, Dar es Salaam.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Risper Koyi (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa wadau kuhusiana na Mikataba ya Kimataifa ya Usimamizi wa Kemikali.

Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga (aliyekaa katikati) na Mkemia Mkuu wa  Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto, waliokaa) wakiwa pamoja na wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es  Salaam .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...