Na Woinde Shizza Globu ya jamii ,Arusha
WATALAAM wa manunuzi ya umma nchini wametakiwa kuzingatia weledi katika utendaji wao wa kazi na kuepukana na vitendo vya ubadhirifu ,rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hiyo itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kusaidia fedha hizo kutumika katika maendeleo mapana zaidi ya Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu na wabobezi wa manunuzi ya umma(IPPC) kutoka nchini 46 duniani unaofanyika jijini Arusha nchini Tanzania,Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philp Mpango amesema mkutano huo unalenga kujadiliana namna ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia taknolojia mpya ya manunuzi .
‘’Ununuzi wa umma ndio sehemu kubwa ambapo fedha za bajeti zinapita, hivyo ukifanyika vibaya maana yake Serikali inapata hasara ndio maana tunasisitiza weredi wa wataalamu wa manunuzi kwa sababu kuna mamunuzi hewa na miradi hewa,"amesema.Aidha amesema asilimia 70 ya fedha za matumizi ya kawaida zinapitia ununuzi wa umma na asilimia 100 ya bajeti ya fedha zote za maendeleo zinapitia manunuzi ya umma ,hivyo bajeti zote katika maeneo hayo mawili zikitumika vibaya lazima serikali iumie.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya manunuzi Dkt. Hellen Bandiho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabobezi na wanunuzi wa umma jana ,uliofanyika katika ukumbi wa simba uliopo ndani ya jengo la mikutano la AICC .
Dkt Mpango akifungua mkutano wa siku tatu unaohusu bodi ya manunuzi, jana jijini Arusha
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutao huo
waziri Dkt Mpangao akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya taasisi ya wizara ya fedha na mipango(picha zote na Woinde Shizza,Glob ya jamii Arusha.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...