Na.Vero Ignatus Arusha. 

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama amewataka Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji ili waondokane na tatizo hilo na kujikita kwenye maendeleo. 

Waziri Mhagama ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 25 ya maonyesho ya kilimo na mifugo nane nane kanda ya kaskazini jijini Arusha.
Amewataka viongozi hao kutatua migogoro hiyo ili kukuza sekta hizo kwani lengo la serikali ni kuhakikisha matumizi bora ya ardhi yanafanikishwa ili kuongeza tija za kiuchumi. 

Mhe. Jenista amesema kuwa migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji inachangia kuzorotesha ustawi wa jamii kutokana na migogoro hiyo hivyo viongozi hao wahakikishe wanakomesha tatizo hilo. "Sekta hizo zinatakiwa kuungwa mkono na kuachana na migogoro hiyo ya muda mrefu ambayo haina tija kwa jamii zaidi ya kusababisha mtafaruku na uvunjifu wa amani," alisema. 

Alisema pamoja na kuyafunga maonyesho hayo rasmi yenye kauli mbiu ya wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda, lakini yataendelea kwa siku mbili zaidi Agosti .Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kilimo na mifugo ndiyo sekta zinazoshikilia uchumi wa wananchi wengi kanda ya kaskazini hivyo wataendelea kuwaunga mkono wanaojishughulisha na sekta hizo. 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwila alisema wakulima na wafugaji wakitumia elimu waliyoipata kwenye maonyesho hayo watanufaika kiuchumi. Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alimpongeza Waziri Mhagama kwa hotuba yake na alimuahidi kwa niaba ya Wakuu wenzake wa mikoa kufanyia kazi ushauri uliotolewa. 

"Pamoja na hayo tunakupongeza mno kwani huku kwetu masaini wakishasema mama anachapa kazi hatuna la zaidi la kuongoza zaidi ya kukubalina na hilo hongera sana kwa kuchapa kazi," alisema Mnyeti .Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Hudson Kamoga ambaye mkulima wa eneo lake alishika nafasi ya tatu kwenye maonyesho hayo alisema wataendelea kuwaunga mkono wafugaji na wakulima kwa lengo la kukuza sekta hizo. 

Mkurugenzi wa Bajuta International Ltd, Gesso Bajuta ambaye kampuni yake ilipata ushindi kwenye maonyesho hayo alisema wamejipanga kuendelea kutoa huduma ya dawa za mifugo pembejeo za kilimo kwa wananchi wote.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama, akizungumza na wananchi waliohidhuria katika maonyesho ya wakulima na sikukuu ya nanenane katika viwanja vya TASO Njiro mkoani Arusha. 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Hudson Kamoga akipokea kwa niaba zawadi ya mkulima kutoka Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama, katika halmashauri hiyo aliyeshika nafasi ya tatu, kushoto kwake ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akifiatiwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...