*Ni baada ya walimu kumtuhumu kwa ulevi, rushwa, kughushi nyaraka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Bibi. Pudencis Protas kumkamata Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wa wilaya ya Ruangwa Bw. Anthon Mandai kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walimu wakimlalamikia kiongozi huyo kuwa na tabia za kudai rushwa, kutowapandisha madaraja, ulevi pamoja na kuwaita walimu hao kwenye vilabu vya pombe kwa ajili ya kuwasikiliza matatizo yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Agosti 12, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika siku ya mwisho ya ziara kyake ya kikazi wilayani hapa. Bw. Mandai anakaimu nafasi hiyo tangu Juni, 2012.

Amesema mbali na kulalamikiwa na walimu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ulevi na kuwaita walimu katika vilabu vya pombe pindi wanapohitaji kuhudumiwa, pia amekuwa akighushi nyaraka za mirathi, jambo linalosababisha baadhi ya familia za waliokuwa walimu kuchelewa kupata haki zao.

“Huyu Katibu ameshindwa kuwasaidia walimu katika kutatua changamoto zao na badala yake amekuwa akitumia vibaya majina ya viongozi wakuu, ambapo hata mimi alijaribu kutaka kunichakachua kwa kughushi muhtasari wa kikao cha mirathi ya Mwalimu Suwedi Chikawe akitumia jina langu kuwa nilikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa na agenda ya kumbadilisha msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na familia jambo ambalo si la kweli,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Fadhili Juma, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Anthon Mandai, akipanda gali la Polisi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudencis Protas, kumkamata ili akajibu tuhuma zinazomkabili, Agosti 12.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...