WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi. 

Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine. Hatua ya kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo. 

Akizungumza namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4 ambazo wameweza kununua madawati 40 na viti “Mh Saida umetenda wajibu wako ipasavyo maana taarifa ya mkuu wa shule inasema kuna uhaba wa viti 163ubawa wa meza 100 hivyo kupatina kwa hivyo vilivyokabidhiwa leo kumepunguza nusu lakini nitaendelea kushirikiana nanyi “Alisema 

“Kazi nzuri inafanywa kwenye shule ya sekondari Chumbageni na nimeambiwa kiwango cha ufaulu kinaongezeka mwaka hadi mwaka asilimia 51 hadi asilimia 77 lakini pia nitoe pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutatua changamoto ya elimu sio watu kusubiri mpaka serikali kuu kwani wamekuwa wakijiongeza na diwani Saida kutatua changamoto ya elimu kwenye kata yake “Alisema. 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash 
AWAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akiwa amekaa kwenye mmoja ya madawati 40 aliyoyakabidhi leo kwa shule ya Sekondari Chumbageni kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi ambaye alimuomba Waziri huyo madawati hayoi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwakabidhi madawati hayo 
 Sehemu ya madawati na viti ambayo yamekabidhiwa leo na Waziri Ummy kwa shule ya Sekondari Chumbageni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...