SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema kwamba kutoka mwaka 2010 imeingiza katika uchumi wa Tanzania zaidi ya dola za Marekani milioni 278 kutokana na huduma mbalimbali inazotoa kusaidia wakimbizi ambao wapo nchini.

Aidha fedha hizo zimeingia katika mfumo wakati Tanzania inatumika kama kituo cha lojistiki kusaidia maeneo mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki wenye matatizo.

Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya Siku za msaada duniani, inayokumbukwa kuadhimisha mauaji ya watoa misaada wakati wa mashambulio ya anga ya Baghdad, Irak miaka kadhaa iliyopita.

Aidha siku hiyo inaadhimishwa Agosti 19 kila mwaka kutoa neno kwa jamii ya dunia kuwakumbuka watoa misaada ambao wapo katika hatari ya maisha kutokana na vurugu zinasumbua duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Tanzania, Michael Dunford alisema kwamba kumekuwepo na uingizaji mkubwa wa fedha katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa na kusaidia chakula kwa wakinbizi waliopo nchini Tanzania kwa kusaidiana na mashirika mengine.

Kwa Tanzania kwa sasa inahifadhi wakimbizi 297,000 kutoka Burundi na Kongio (DRC) katika maeneo ya Nyarugusu, Nduta na Mtendeli mkoani Kigoma .
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael. Dunford.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...