Na Agness Francis,Blogu ya Jamii.

BARAZA la sanaa la taifa limetoa ufafanuzi wa kanuni za baraza hilo zitakazokuwa zinatumika kuendeshea kazi za sana hapa nchini.

Kanuni hizo zilizoanza utekelezaji wake mwaka huu katika kusimamia shughuzi zote zinazohusiana na sanaa.Akifafanua kanuni hizo Afisa Sana Basata Augustino Makame leo katika ofisi zao Jijini Dar ea Salaam amesema kuwa badhi ya sehemu za kanuni hizo zimebainishwa.

Ambazo ni muundo wa baraza,usajili na vibali vya kazi,uwasilishwaji wa taarifa kwa msajili,kufutwa kwa usajili,masharti ya jumla kwa wadau wa kazi za sanaa,masharti ya jumla ya kazi za sanaa,makosa na adhabu,uzingatiaji wa sheria katika kazi za sanaa.

Afisa huyo amesema baraza ndilo litakalokuwa msajili mkuu na mtoa vibali vyote vya kufanya kazi zsanaa kwa wasajili."Msajili atato kibali na kitambulisho cha kufanya kazi za sanaa kwa mtu au kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa kanuni hizo,amesema makame"

Aidha Makame amesema mtu yoyote hatoruhusiwa kufanya kazi za sanaa bila kusajiliwa na baraza au upelekwa sokoni ama kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitishwa kuwa na maudhui na madili kuzingatiwa,ambapo kibali kitalipwa kila mwaka kwa mujibu wa ada zitazolipwa katika halmashauri husika. Vile vile amesema shughuli zote zinazohusiana na sana zitafanyika kwa kuzingatia sheria zote za jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kanuni zake.

Makame amemalizia kwa kusema kuwa endapo kazi ya msajili yeyote itakiuka masharti ya kanuni hizo msajili huyo atachukuliwa hatua na baraza kwa mujibu wa kanuni 64 (1) au (2),itakuwa ni kosa la jianai na kwa mtandao wowote ama chombo chochote cha habari kurusha kazi hiyo kwa namna yoyote ile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...