Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimehitimisha kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa kuwahakikishia wananchi yote yaliyoahidiwa yatatekelezwa na hakuna wa kuwarudisha nyuma.

Wakati wa kuhitimisha kampeni hizo leo mamia ya wananchi wa Jimbo la Ukonga wamejitokeza kwa wingi huku Katibu Mkuu wa CCM  Dk.Bashiru Alli akiweka wazi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk.John Magufuli amefanikiwa kudhibiti ugonjwa uliokuwepo wa baadhi ya wanachama  kutumia rushwa ili kupata uongozi

Akizungumza mbele ya maelfu ya  wananchi wa jimbo hilo Dk.Bashiru amewaomba wamchague mgombea ubunge wa CCM Mwita Waitara kwani ndio mtu sahihi huku akieleza namna ambavyo Chama hicho kimejipanga katika kuwatumikia wananchi hasa katika kuwaletea maendeleo. Ameeleza miradi  namna mikubwa ya maendeleo inavyoendelea kutekelezwa na kwamba anawashangaa wanaodai uchumi umedorora.

Hivyo Dk.Bashiru amewaomba wananchi hao kumchagua Waitara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika suala la maendeleo. Pia amewahakikishia waliohamia CCM kwamba wote  wana haki zote za uwanachama na hakuna ubaguzi na kuwahakikishia kwa namna ambavyo wamejipanga waliohamia na watakaoendelea kuhamia hawataondoka tena.

Amewaambia wananchi kwa sasa CCM kuna mambo kadhaa yanayofanyika ili kiendelee kuwa imara zaidi.Ametaja baadhi ya mambo hayo ni  kuwa na sauti moja kati ya Serikali na Chama.Pia wanaimarisha umoja ndani ya chama hicho.

"Moja ya changamoto ya kufa kwa upinzani ni kukosekana kwa umoja na CCM tumegundua hilo na ndio maana tumeamua kuimarisha umoja na mshikamano," amefafanua.

Pia amesema CCM imebadilika tofauti na hapo nyuma ambapo kulikuwa na tabia ya kupanga safu na vyeo lakini sasa ugonjwa huo umepona na aliyeutibu ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk.John Magufuli.

Dk.Bashiru ametoa onyo kwa watendaji wenye tabia ya kuwa na wagombea wao na atakayebainika atamfukuza na kwamba huu si wakati wa kubeba wagombea wala kupanga safu kwani wanachama wote ni sawa.

"Muda wa kutafuta vyeo haujafika na kwamba hatutaki yaliyotokea mwaka 2015 wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu yarudie.Wanaotembea na wagombea wao nitawachukulia hatua kwani hilo lipo ndani ya uwezo wangu," amesema.

Wakati huo huo amesema wapo wanaodai kwamba CCM hawakufuata utaratibu kumpata mgombea wake lakini ukweli taratibu zote zimefuatwa ambapo ikiwa pamoja na mgombea kuchukua fomu kwa Katibu wa Wilaya na kisha mchakato wote kuendelea kwa utaratibu uliopo. Hivyo amewaomba wananchi katika uchaguzi wa kesho wahakikishe wanamchagua mgombea wa CCM.
Kwa upande wake Waitara amewaomba wananchi wa Ukonga wampigie kura na lengo lake ni kuwa mbunge ambaye atakuwa na jukumu la kuzungumzia maendeleo ya jimbo hilo na atakuwa na nafasi sahihi ya kuzungumza maendeleo.
Pia amesema wapo wanaosema amenunuliwa,hivyo anataka kuwathibitishia Chadema kwamba hajanunuliwa huku akieleza namna ambavyo CCM ilivyokuwa na mpangilio wa kutekeleza mambo yake.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akimnadi  mgombea wa  ubunge  CCM,Mwita Waitara ambapo amewaomba wananchi aajitokeze kwa wingi na kumpigia kula mgombea wa CCM.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongizi wa chama hicho na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za uchanguzi jimbo la Ukonga ambapo  amewaomba wa wananchi wamchague mgombea wa ubunge wa CCM,Mwita Waitara.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na wananchi wa Ukonga katika ufungaji wa kampeni za uchaguzi ambapo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura  na kumchngua kiongozi anao ataowaletea maendeleo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwapokea wanancha waliotoka vyama vya upinzani






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...