Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) inadaiwa zaidi ya sh. Bilioni Moja na Bodi ya Bonde la Wami/ Ruvu ikiwa ni kusambaza maji bila kulipia bonde kwa ajili ya uendelezaji wa vyanzo vya maji. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa baadhi ya mamlaka za maji katika mikoa wanatumia bonde la Wami/ Ruvu wamekuwa wakilipa vizuri isipokuwa Dawasa. 

Amesema kuwa licha ya Dawasa kuwa na mikakati ya usambazaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam hivyo lazima walipe katika bonde kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji hivyo. 

Ngonyani amesema kuwa maji ambayo wananchi wanapata yanatokana na kuwepo vyanzo vya maji ambavyo vinahifadhiwa na mamlaka zilizopo kazi yake ni kusambaza tu. 

Amesema kufikia deni hilo kwa Dawasa ni kutokana na kila wakipelekewa Ankara zao wanazichukua na kuzihifadhi huku wakiendelea kutoa huduma za maji. 

Amesema kuwa wenye visima wote katika jiji la Dar es Salaam wafike katika ofisi za Bodi ya bonde la Wami/Ruvu kupata amelezo juu ya ulipaji wa Ankara za maji ndani ya mmoja baada ya hapo watapita kwa kila watu wenye visima. 

Aidha amesema kuwa kampuni za uchimbaji wa visima watakutana nao Oktoba mwaka huu kwa ajili ya kupeana maelezo katika uchimbaji wa kisima. 

Ngonyani amesema ada ya uchimbaji wa kisima ni sh.150,000 na baada hapo kupewa utaratibu wa ulipaji wa ada kwa kila mwaka kuendana na matumizi. 
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kazi za bonde la Wami/Ruvu pamoja na kuzikumbusha Mamlaka za Maji kulipa Ankara zao , jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...