Na Mathias Canal-WK, Dodoma
Katika
vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania masoko ya Kahawa yamekuwa
yakiendeshwa kwa mfumo wa ushirika na soko huria, Mfumo wa soko huria uliruhusu
makampuni na watu binafsi kununua mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima
pasipo udhibiti hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo bei
isiyokuwa na tija kwa mkulima, ubora hafifu wa mazao, ukwepaji wa kodi kwa
wanunuzi na ukosefu wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo.
Kutokana
na changamoto za mfumo wa soko huria, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli iliamua
kurejesha ununuzi wa mazao matano ya kimkakati (Korosho, Tumbaku, Pamba,
Kahawa, na Chai) kupitia vyama vya ushirika tangu mwaka 2016 ili kunufaisha
wakulima, wanunuzi/wafanyabiashara na serikali.
Hayo
yamebainishwa jana tarehe 14 Septemba 2018 na Mhandisi Mhe Dkt Charles Tizeba,
Waziri wa kilimo wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa
nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika
ukumbi wa mikutano wa CCM Makao makuu maarufu kama White House, Mkutano
uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga, Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Makongoro Nyerere, Naibu
waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba, wataalamu kutoka wizara ya kilimo akiwemo
Naibu katibu mkuu Prof Sizya Tumbo, Mrajis wa vyama vya ushirika,vyama vya
ushirika na wawakilishi wa wakulima kutoka maeneo yanayolima kahawa.
Katika
taarifa hiyo Dkt Tizeba alieleza kuwa kamwe hawezi kuruhusu mtu mmoja mmoja au
kundi la watu kuvunja ushirika ambao hivi karibuni umeanza kuimarika mahususi
kwa ajili ya kumkomboa mkulima uamuzi ambao umebainishwa kwenye ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 katika sura ya pili ibara ya
22 ikisisitiza kuviimarisha na
kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya
wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na
uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji wa thamani na
biashara.
Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo akitoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Washiriki wa mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akizungumza mara baada ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo kutoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Wataalamu kutoka wizara ya kilimo wakifatilia mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...