Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha.

Vita dhidi ya ujangili wa Faru, imeendelea kushika kasi na sasa Faru wa serengeti,wataanza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika mradi ambao utagharimu zaidi ya 2.5 bilioni

Mradi huo,unafadiliwa na shirika la uhifadhi za Friedkin conservation Fund(FCF) kwa kushirikiana na shirika la Frunkfurt zoological society na kusimamiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini(TANAPA) na taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI).Mratibu wa Mradi wa uhifadhi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Philbert Ngoti alisema, vifaa hivyo ambavyo vitawezesha Faru wa Serengeti kuwa salama zaidi.

Alisema Faru wa Serengeti wanafungwa vifaa vya aina mbili,vya kielekroniki VHF transmitter ambacho kinawezesha kuwafatilia walipo kila siku na pia wanafungwa katika mguu wa kulia kifaa cha kisasa cha LoRa collar ambacho pia kinafatilia na kuonesha mienendo yao kila siku.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga, alisema zoezi la ufungwaji wa vifaa ya utambuzi na usalama kwa Faru ni muhimu sa katika kuimarisha vita dhidi ya ujangili.

Alisema zoezi hilo pia litasaidia kuongeza ufatiliaji wa faru,wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani na sasa kila siku watajulikana wapo wapi, wanakula nini, wanaumwa ama wanamatatizo na hivyo kuchukuliwa hatua.
Meneja miradi wa shirika la Frunkfurt Tanzania, Rian Habuschagne, alisema katika mradi huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika nchini, pia kumejengwa minara ya mawiliano katika maeneo yote ya mapito ya Faru.

Alisema zoezi la kufungwa vifaa hivyo linasimamiwa na watafiti na wahifadhi maarufu wa Faru barani Afrika, wakiongozwa na Pete Morkel na wanatarajia Faru wote wa serengeti kufungwa vifaa hivyo."hili zoezi linagharama kubwa tunawashukuru Friedkin Conservation Fund kwa msaada mkubwa wa fedha na helkopta, pia Frunkfurt ,TANAPA na taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI)"alisema.HIfadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maeneo yenye Faru wengi kwa sasa hapa nchini kutokana na kuimarishwa ulinzi

Picha naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Japhet Hasunga akiwa anashikiri zoezi la kuwafunga Faru wa serengeti vifaa vya ulinzi na mawasikiano
 
  Faru wa serengeti wakianza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika mradi ambao utagharimu zaidi ya 2.5 bilioni 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...