TAASISI isiyo ya kiserikali (NGOs) ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema (Good Deeds Day) ambayo kidunia itafanyika Aprili 7,2019.


Siku hii ya matendo mema itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali pamoja na huduma kwa watu wenye mahitaji katika jamii.



Akizungumza katika uzinduzi wa siku ya matendo mema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye pia amechaguliwa kuwa mlezi wa Marafiki Tanzania Charity amewaomba wananchi kujiunga na Marafiki Tanzania Charity ili kuweza kufanikisha kuchangia vitu mbalimbali ikiwa pamoja na huduma kwaajili ya wahitaji katika jamii yetu.


Pia Makamba amewaomba wanamarafiki Tanzania Charity kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka kwa kila mtanzania ili kuongeza wana marafiki Tanzania kuwa wengi zaidi.

Nae Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi-Sinza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Padre Josephat Mhozya amehamasisha kila mtu kutenda matendo mema.

"Kutenda matendo mema ni Ibada kwahiyo watanzania tutende matendo mema kwakuwa tukitenda matendo mema tutalipwa na mwenyezi Mungu" Amesema Mhozya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini. Uzinduzi huo umefanyika na tasisi isiyo ya kiserikali (NGOs) ya Marafiki Tanzania Charity iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Marafiki Tanzanua Charity, Emmanuel Makundi akizungumza katika uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya wahitaji pamoja na huduma ambazo zinahitaji na wahitaji mbalimbali hapa nchini.
Mratibu wa Good Deeds Day Tanzania, Doroth Namuhisa
 akizungumza katika uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamarafiki Tanzania Charity na watu mbalimbali waliohudhulia uzinduzi wa siku ya Matendo Mema. Siku ya matendo Mema tafanyika Aprili 7, 2019 duniani kote.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akiwa katika picha ya Pamoja na wanamarafiki Tanzania Charity mara baada ya kumaliza uzinduzi wa siku ya Matendo Mema (Good Geeds Day) uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa amikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...