LUSUNGU HELELA-DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu

Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi ameelezea kufurahishwa kwake na ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi wa Wizara hiyo na kuelezea kuwa, ndio umemwezesha kuiongoza vema wizara hiyo kwa kipindi alichokuwepo madarakani na kupelekea mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Wanyamapori, Utalii, Misitu na Nyuki na Malikale.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya ujangili ambayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliopatikana kutoka kwa watumishi wa Wizara, wananchi, Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa Wanyamapori.

“Katika Kipindi tulichokuwa pamoja, kuna mambo mengi tumeyakamilisha. Nimefanya kazi nanyi na kila mmoja wenu alikuwa akinisaidia ili Wizara yetu iweze kusonga mbele. Hakuna hata mmoja aliyeonyesha kutaka kunikwamisha. Ninawashukuru sana”Amesema Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa UDOM jijini Dodoma na kuhudhuriwa na watumishi wapatao 113 wa Wizara hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aloyce Nzuki, amempongeza Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi kwa kustaafu rasmi jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kulia) akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki.
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili wakiwa wamesimama kwa muda wa dakika moja mara ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara kabla ya kuzungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kwa ajili ya kuwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu. .
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) mara baada kumaliza kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( wa pili kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (wa kwanza kushoto) akiwasili kwa ajili ya kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Wengine ni Wasaidizi wake. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...