Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka, akisisitiza jambo kwa wasindikaji wa vyakula (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uzalishaji bidhaa hizo. Kutoka kushoto, waliokaa ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Niombe, Dkt. Buni Mwakasage (wa kwanza) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa; Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA Makao Makuu, Bw. Justin Makisi (wa pili); Meneja wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Rodney Alananga (wa nne); na Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Bi Mariam Smalling (wa tano).
 Picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Njombe, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika Ufunguzi wa mafunzo hayo. Waliokaa kutoka kushoto ni Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka (wa tatu), Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA Makao Makuu, Bw. Justin Makisi (wa pili); Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Bi Mariam Smalling (wa kwanza); Mganga Mkuu wa Mkoa wa Niombe, Dkt. Buni Mwakasage (wa nne) ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa; Meneja wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Rodney Alananga (wa tano); na Mkaguzi Mkuu wa Chakula kutoka TFDA Makao Makao Makuu, Bw. Lazaro Mwambole (wa sita).
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia mada katika mafunzo hayo ya usindikaji vyakula mkoani Njombe.
                                                    
Na:  James Ndege - Njombe
TFDA imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo 120 wa usindikaji wa vyakula mkoani Njombe kwa lengo la kuwezesha ukuaji wa Sekta ya  viwanda nchini vinavyokidhi vigezo vya usalama na ubora ili kupata soko la ndani na nje ya nchi hivyo kukuza uchumi wa jamii na Taifa.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kibena kilichopo mjini Njombe kuanzia tarehe 25 – 26 Septemba, 2018 ambapo wasindikaji 120 kutoka katika Hamlshauri sita (6) za Njombe Mji, Njombe Halmashauri, Makambako, Wanging’ombe, Ludewa na Makete walishiriki.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka.

 alisema “Ninafurahi kuona TFDA leo wanatoa mafunzo haya muhimu ili ninyi wasindikaji wa mkoa wangu muweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo vingi vitakavyochakata mazao yetu na kuongeza thamani ya bidhaa hizo. Jambo hili litafanya mkoa wetu uinue kipato cha wananchi wake na Taifa kwa ujumla, hivyo zingatieni mafunzo haya na uongozi wa mkoa utashirikiana nanyi katika kutatua changamoto zenu ili malengo yetu ya kuwa na viwanda vinavyokidhi vigezo yaweze kufikiwa”.

Aidha, Mgeni Rasmi katika kufunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA Makao Makuu, Bw, Justin Makisi aliwapongeza wasindikaji hao kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo na kuwaasa kuzingatia ushauri wa wataalam katika kuzalisha bidhaa zao ili ziweze kusajiliwa na TFDA hivyo kupata soko la ndani na nje ya nchi.

 “Nakabidhi maazimio yenu katika uongozi wa Mkoa uliopo hapa sasa ili yale yanayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali katika ngazi ya Mkoa yafanyike, nanyi wasindikaji mna wajibu wa kutekeleza yanayowahusu ambapo tukishirikiana kwa pamoja, suluhisho la changamoto hizo zitabadilika kuwa fursa. Ofisi ya TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja waratibu wa majukumu ya TFDA katika Halmashauri zenu wapo nanyi siku zote hivyo watumieni kupata huduma na ushauri mara kwa mara” alihitimisha kiongozi huyo.

Katika mafunzo hayo, TFDA ilishirikisha Taasisi nyingine za Serikali za Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na BRELA ili kuwawezesha wasindikaji hao kutambua mambo muhimu yanayotakiwa katika kuzalisha bidhaa zinazokubalika kwa mujibu wa sheria zilizopo. Mafunzo hayo ya TFDA ni endelevu na mkoa wa Njombe umekuwa mkoa wa 22 nchini kupata mafunzo ya aina hiyo.                                                          

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...