Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameutahadharisha umma wa jiji la Dar es salaam kuhusiana na utapeli wa nyumba hasa kwa baadhi ya watu kutumia hati wasizo na miliki nazo kuomba mikopo mikubwa katika benki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makonda amesema "baadhi ya watu hukopa fedha na kuacha hati zao za nyumba kama bondi lakini wale walioachiwa hugeuka na kutumia hati hizo kwa kuomba mikopo mikubwa katika mabenki na wakishindwa kulipa watu wasiohusika na madeni hayo huusishwa hasa kwa nyumba zao kuuzwa" amesema Makonda. Sambamba na Makonda amempongeza Waziri ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi kwa kusimamia suala la hati za kidigitali ambazo huweza kutambua hati kieletroniki.

Aidha ameeleza kuwa wale wote wenye mikopo wasiyoielewa katika mabenki mbalimbali kuanzia jumatatu wakaripoti kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya na baadaye Seeikali ya Mkoa itakutana benki zote 56 na kujadili suala hilo ambalo linaibia mabenki na kupoteza mali na haki za makazi kwa wananchi.

Pia amewataka Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam hasa wa Wilaya ya Kinondoni ambako kuna kesi zaidi ya 500 za watu kuuziwa nyumba zao bila kutokuwa na mikopo katika mabenki kutumia nafasi hiyo ili kuepuka kughudhibiwa na kufilisiwa mali zao na amewashauri wananchi kuwa makini kwa kutunza hati hizo.

Kuhusiana na uchaguzi wa marudio unaotarajia kufanyika kesho katika jimbo la Ukonga na kata 2 jijini humo Makonda amesema kuwa uchaguzi huo utakuwa wa amani kwani kamati ya ulinzi na usalama imejipanga vyema hivyo wananchi wasiwe na shaka wafuate taratibu na baada ya uchaguzi washangilie kwa amani bila fujo ili kulinda amani ya jiji ambalo ni kitovu cha biashara na utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...