Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa taarifa ya kampeni ya usafi iliyoanza takribani mwezi mmoja uliopita katika kikao kilichohusisha wadau ya afya na mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho Makonda amesema kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo zaidi ya watu 1,0000 wamekamatwa, watu 4443 waliachiwa huru, 376 walipata dhamana na takribani watu 6577 walilipa faini iliyofikia shilingi milioni 346 na laki 6 ambapo nusu ya fedha hizo ilikuwa ni malipo kwa mgambo wanaosimamia usafi na hadi sasa watu 6 bado wapo mahakamani.

Aidha amesema kuwa yeye na wakuu wa Wilaya wamelaani kitendo cha mgambo wa kusimamia usafi kumpiga raia katika eneo la Bunju na wamefatilia na hadi sasa watuhumiwa wapo katika gereza la Segerea na amewataka mgambo hao kufanya kazi kwa kufuata na kusimamia sheria kwani hakuna sheria inayorusu kupiga raia.

Aidha amewashukuru wadau na wananchi hasa wale wanaofanya usafi bila shuruti na kuwataka Wakandarasi kufanya kazi kulingana na mikataba yao na kwa kampuni zilizodanganya katika mikataba yao wajiandae kulipa gharama hizo kwa serikali.

Sambamba na hilo Makonda amewataka wanajamii wa jiji la Dar es salaam kushiriki katika shughuli za usafi na kila mmoja wa nafasi yake ashiriki suala hilo na wao kama serikali ni wasimamizi na wawezeshaji na amewataka wafanyabiashara na wenye viwanda kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Pia Mkuu wa Mkoa ameeleza changamoto za mchakato huo ni pamoja na uchache wa watendaji na uchache wa mashine za EFD na ameeleza kuwa zoezi hilo ni endelevu katika kuhakikisha jiji linakuwa safi.

Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Abubakar Kunenge amesema kuwa suala la usafi ni wajibu wa kila mmoja na hakuna chaguo zaidi ya kuhakikisha jiji linakuwa safi na usafi ufanyike bila shuruti na uwe tabia ya kila mmoja na amewaomba wadau wa afya na mazingira kuhamasisha katika suala zima la mazingira.

Mkutano huo umeshirikisha wadau na taasisi mbalimbali za mazingira na kujadili namna ya kuweka jiji katika hali bora zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es SalaamPaul Makonda akizungumza leo na wadau mbalimbali wa usafi katika ukumbi wa Anatoglo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

 Sehemu ya wadau mbalimbali wa usafi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...