Seif Mangwangi,Arusha
NCHI za Afrika zitaendelea kukabiliwa na uhaba wa mbegu bora za msingi zenye kutoa mazao mengi na bora kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo kuwa mdogo kulinganisha na mahitaji halisi.

Hali hiyo itaendelea kusababisha uzalishaji wa vyakula kuwa wa chini na hivyo kushindwa kukabili tatizo la njaa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika mara kwa mara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha mbegu za msingi ya Quality Basic seed yenye makao yake mkuu nchini Kenya, Wycliffe Ingoi amesema mahitaji ya mbegu bora za msingi ni kilo 156250 kwa mwaka.

Amesema kiwango hicho ni kikubwa kutokana na ugumu wa kuzalisha mbegu hizo sanjari na uwepo wa kampuni chache zinazoweza kuzalisha mbegu hizo.

" Wakulima wamekuwa wakipata mazao machache kutokana na uhaba wa mbegu za msingi na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizo na ubora na ambazo hazijazalishwa kitaalam, sisi kama QBS tumekuja kujaribu kumaliza hili tatizo japo kwa kiasi fulani,"amesema.

Aliziomba Serikali za Afrika kushirikiana na kampuni zinazozalisha mbegu za msingi  ili kufanikisha zoezi la kupatikana kwa mbegu bora na zenye kutoa mazao mengi.

kwa upande wake Ofisa Habari wa taasisi ya kilimo ya African Agriculture Technology Foundation (AATF),inayosaidia kusambaz teknolojia ya kilimo Afrika, Everlyne Situma alisema kampuni za mbegu zimekuwa zikishindwa kuzalisha mbegu za kutosha kutokana na ugumu wa kutayarisha mbegu za msingi.

Amesema kampuni ya Quality Basic Seed imekuwa mfano wa kuanzisha utaalam huo na hivyo kuwa msaada kwa kampuni za uzalishaji wa mbegu Afrika.
Meneja masoko wa kampuni ya kuzalisha mbegu za awali ya Quality Basic Seed, Cliffe ingoi akiwaeleza waandishi wa habari namna kampuni yake inavyofanya uzalishaji wa mbegu hizo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...