Na Asha Ngoma
Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma wameadhimisha miaka 51 tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 1967 katika hotel ya Serena Hotel jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2018.
Hata hivyo sherehe hizo hazikuwa na shamrashamra zilizoandaliwa na badala yake ukafanyika mkutano na wanahabari baada ya kuahirisha sherehe hizo kutokana na maombolezo ya kitaifa ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere huko Ukara, Mkoani Mwanza.
Tanzanite Founder Foundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali lilioanzishwa na kusajiliwa mwaka 2013 ikiwa na lengo kuu la kuwajengea uwezo vijana na watu wote waishio migodini na maeneo jirani ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku kutokana na madini haya.
Tanzanite Founder Foundation na wadau leo
imeona iadhimishe miaka 51 tangu madini haya ya kipekee duniani kuvumbuliwa nchini Tanzania.
Madini haya husheherekewa ulimwenguni na mashirika, taasisi na wafanya biashara Mbalimbali wa madini lakini hayajawahi kusherehekewa wala kuadhimishwa nchini Tanzania. Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation imeona iadhimishe siku hii kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu madini haya ikiwa ni pamoja na kutoa historia fupi ili kutoa tathmini ya tulipotoka na tulipo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kudhihirishia ulimwengu kuwa Tanzanite ni fahari yetu na urithi wetu watanzania.
Madini ya Tanzanite yalivumbuliwa mwaka wa 1967 na Mzee Jumanne Mhero Ngoma ambaye ni Mtanzania, a iyaokota madini haya katika eneo la Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Arusha wakati huo na kuyapeleka kwa ofisi ya Madini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ambayo nayo hawakuyatambua ni madini gani.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akiwa na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma (wa pili kushoto) na watendaji wa taasisi hiyo katika mkutano na wanahabari katika kuadhimisha miaka 51 tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 1967 huko Mirerani. Mkutano huo umefanyika leo katika hotel ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akipongezana na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akiwa na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma. Kusoma habari kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...