Na Wankyo Gati, Arusha

Shirika la umeme Mkoani Arusha TANESCO limekamata Zaidi ya nguzo kumi na saba kwa kipindi cha miezi sita ambazo zimekuwa zikiwekwa na vishoka ambao wamekuwa wakijihusisha na wizi wa miundombinu ya umeme katika maeneo ya Murieti na Usa riva Mkoani Arusha.

Ambapo amesema kuwa vitendo vyaa uharibifu wa miundombinu ya umeme tanesco yamekuwa yakishika kasi siku hadi siku licha ya oparesheni zinazofanywa za kukamata vishoka hao bado changamoto hiyo imekuwa ikishindikana kupatikana ufumbuzi juu suala hizo.

 Hayo yameeelezwa leo Afisa usalama wa shirika la umeme  tanesco Arusha Dominic Nerrey wakati wa kuendesha opereshen ya kuondoa nguzo zote ambazo haziko kwenye raman ya umeme wa shirika hilo ili kuweza kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi katika eneo la Murieti katika jiji la Arusha.

Aliongeza kuwa  kuwa oparesheni ya kukamata na kuwafikisha katika mikono ya sheria ili uweza kukomesha viteno hivi ambavyo vimekuwa vikilitia shirika hasa kubwa vishoka wanaohujumu shirika hilo imefanywa kwaajili ya kuondoa nguzo ambazo hazipo kwenye ramani ya umeme wa shirika hilo lengo likiwa ni kuboresha huduma mbalimbali za upatikanaji wa umeme Mkoani Arusha


K wa upande wake afisa uhusiano huduma kwa wateja kutoka tanesco A rusha Said Mndeme amesema kuwa wahujumu miundombinu ya tanesco wamekuwa wakitia hasara kubwa sana hususan kuharibu line za umeme ambao zimekuwa zinzpeleka huduma za umeme kwa wananchi ambapo hali hiyo imekuwa ikisababisha kupata umeme mdogo kwa baadhi ya maeneo wanayotoa huduma.


 Nae meneja wa tanesco Mkoa wa Arusha Henry Mhina  hapa anakiri kuwepo kwa vishoka hao ingawa anasema hali hiyo inachangiwa na wananchi wenyewe kutokwenda kupata huduma za kuunganishiwa umeme katika shirika hilo.

Aidha anaongeza kuwa zipo sababau mbalimbali zinazotajwa kuendelea kuwepo kwa ongezeko la vishoka hao ikiwemo uwepo wa miradi ya umeme inayotekelezwa katika nyakati tofauti ikiwemo mradi wa wakala wa umeme vijijini REA,Pamoja na Tanesco wenyewe ambapo katika maeneo ya Murieti mradi uliishia decemba 2017 huku eneo la Murieti likiwa ndiyo Korofi dhidi ya Vishoka hao.

Kwa niaba ya wananchi wenzao Mery Maliwa na Ndetakashulo Ismail  ambapo ndipo kulipokithiri uwepo wa vishoka hao ambapo wanasema wanashangazwa na hali hiyo ingawa ujio wao wanakuja majira ya usiku na kusimika nguzo hizo za umeme na kwamba hii itasababisha wananchi kupata hasara pamoja na kukosa nishati ya umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...