Na Tiganya Vincent
JUMLA ya wanawake 46,158 mkoani Tabora wamejifungua katika kipindi cha kuanzia Januari hadi kufikia Septemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu wa Afya wa Mkoa wa Tabora Tausi Yunge wakati wa mkutano wa wadau wa faya wa Mkoa huo.

Alisema walijifungua chini ya umri wa miaka 20 walikuwa 11,332 ambao ni sawa na asilimia 24.5 na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini waliojifungua walikuwa 34,826 sawa na asilimia 75.4.

Tausi alisema watoto waliozaliwa wakiwa hai walikuwa 45,336 sawa na asilimia 98.7 na wasio hai walikuwa 563 sawa na asilimia 1.2.

Kaimu Katibu Afya Mkoa huyo alisema jumla ya wanawake waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma walikuwa ni 43,991 sawa na asilimia 95.3.

Wakati huo huo Kaimu Katibu huyo wa  Afya Mkoa amesema kuwa hadi hivi sasa ni Wazee 32,470 sawa na asilima 50 ya wazee 71,116 ya waliotambuliwa ndio wameshapewa vitambulisho kwa ajili ya matibabu mkoani humo.

Alisema ni Halmashauri  ya Wilaya ya Igunga ndio inaoongoza kwa kutoa kwa wazee 6,700  kati ya 9,766, kufuatiwa na Kaliua iliyotoa kwa wazee 3,700 kati ya 6,019, Uyui 4,000 kati ya 6,840  na Urambo imetoa kwa wazee 5,120 kati ya 9,387.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kushoto) akifungua mkutano wa wadau wa afya hivi karibuni mkoani humo. Wengine ni  Katibu Tawala Mkoa huo Msalika Makungu( kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(wa pili kutoka kulia) na  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba(kulia)
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba akitoa mada kuhusu hali ya huduma ya afya mkoani humo  hivi karibuni wakati wa mkutano wa wadau wa afya.
 Kaimu Katibu wa Afya Mkoa wa Tabora Tausi Yunge akitoa takwimu za wanawake waliojifungua tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa wakati wa mkutano wa wadau wa afya mkoani humo. 
 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa wadau wa afya mkoani Tabora wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hivi karibuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...