Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI )Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya madereva na makondakta wanaofanya kazi zao katika stendi ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo wakati wa alipofanya ziara yake ya kikazi ya kushitukiza kwa lengo la kusikiliza changamoto ya miundombinu ya vyoo inayowakabili na kuwalazimu kujisaidia katika mifuko ya plastiki pamoja na vichakani .

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

WAZIRI wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefanya ziara ya kushitukiza katika stendi ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo na kubaini kufungwa kwa choo kwa zaidi ya siku tatu bila ya kutumika kutokana na shimo lake kujaa maji  na kupelekea baadhi ya madereva,makondakta pamoja na abiria kupata usumbufu mkubwa na kuamua  kujisaidia katika mifuko ya plastiki aja kubwa na ndogo  na kwenda kuitupa kandokando  ya barabara  na wengine kujisaidia vichakani.

Jafo aliweza  kubaini kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema kwamba katika eneo la stedi hiyo ya mabasi kuna mapugufu mengi katika suala zima la miundombinu ya vyoo,pamoja na kuwepo kwa  miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuwa na  mashimo hivyo kuwapa wakati mgumu madereva katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia waziri Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa maafisa wa mazingira pamoja na afya wa Wilayani Bagamoyo kumwandikia barua ya maelezo kuhusiana na saakata la  kukithiri kwa uchafu huo sambamba na  kumwagiza  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kuunda tume kwa ajili ya kuweza kuchunguza kwa kina kuhusiana na baaadhi ya watu ambao wanafanya hujuma na kusababisha upotevu wa fedha za ushuru wa mabasi katika stendi hiyo.

“Kwa kweli hii hali mimi siwezi kuivumilia kabisa hata kidogo maana nimepata taarifa kwamba stedi hii inachangamoto mbali mbali lakini kubwa zaidi ni kufungwa kwa choo kwa zaidi ya siku tatu kutokana na kuwa ni kibovu, kwa hiyo sasa watu wanaangaika kweli kweli mpaka wanaamua sasa kwenda kujisaidia vichakani na kama haitoshi wengine wanatumia mifuko ya plastiki alafu wanakwenda kitupa hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Jafo.

Kadhalika Jafo aliongeza kuwa kutokana na kukithiri kwa uchafu katika stendi hiyo ya mabasi kunaweza kusaababsiha mlipuko wa magonjwa mbali mbali hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kwa wataalamu wa afya pamoja na mazingira zinafanyike haraka san ili kuweza kukabiliana na hali hiyo ambayo imekuwa ni kero kwa wananchi.

Nao baadhi ya madereva hawakusita kutoa kilio chao  kwa Waziri Japo ambapo wamedai kuwa wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa pindi wanapohitaji huduma ya kujisaidia na kwamba kwa sasa wapo katika mazingira hatarishi ya kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukithiri kwa watu kujisaidia ovyo katika maeneo ambayo sio rasmi.

Aidha katika hatua nyingine Waziri Jafo katika ziara yake hiyo ya kikazi aliweza  kutembelea hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo n akuonyesha masikitiko yake makubwa kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji, na kutoa  muda wa siku 30 kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha  anatekeleza agizo lake alilolitoa la hospitali zote nchini kufunga mfumo wa kielekitroniki wa ukusanyaji wa mapato  unaofahamika kwa jina la Got Homis.

STENDI ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani imekuwa ikilalamikiwa kwa kipindi kirefu kutokana na kuwepo kwa changamoto mbali  mbali zinazoikabili ikiwemo kuwepo kwa miundombinu mibovu ya vyoo,ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji hususan madereva,makondakta pamoja na abiria  na kupelekea kuamua kujisaidia katika maeneo ambayo sio rasmi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...