*Ni kupitia Kongamano la pili la sekta ya mafuta, gesi litalokafanyika Septemba 24/25

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SERIKALI kupitia Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani inatarajia kuzungumzia mwelekeo wa nchi katika kutumia nishati ya mafuta na gesi katika viwanda.

Waziri Kalemani atatoa muelekeo huo katika Kongamano la Pili la Sekta ya Mafuta na Gesi linalotarajia kufanyika kuanzia Septemba 24 hadi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.Mbali ya Waziri kutoa mwelekeo, pia wadau muhimu wa sekta ya mafuta na gesi wakiwamo TPDC, PURA,EWURA, NEEC, ATOGS na TPSF watashiriki.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kongamano hilo Abdulsamad Abdulrahim kutoka Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini amesema Serikali na wadau wa sekta ya mafuta na gesi wameunga mkono na watashiriki kikamilifu.

Amefafanua kongamano hilo limeandaliwa na Pietro Fiorentini Tanzania kwa kushirikiana na CWC Group ambapo pamoja na mambo mengine mradi wa bomba la mafuta ghafi utachambuliwa wakati wa kongamano hilo.

“Mradi huo wa bomba la mafuta unatarajiwa kuleta fursa mbalimbali katika mnyororo wa thamani.Pia kongamano hili litajadili hatua za uendelezaji wa miradi ya gesi iliyopo nchini .

“Miradi ambayo itaifanya Tanzania kuwa mzalishaji na msambazaji mkubwa wa gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki,”amefafanua.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba akifafanua jambo wakati anazungumzia Kongamano la Pili la sekta ya mafuta na gesi litakalofanyika Septemba 24 hadi 25 mwaka huu.
Kamishina Msaidizi wa Mendeleo ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa Kongamano la pili la sekta ya mafuta na gesi

 Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim akizungumza leo kuhusu  Kongamano la Pili la Sekta ya Mafuta na Gesi ambalo litafanyika jijini Dar es Salaam Septemba 24 hadi 25.
Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kongamano litakalofanyika Septemba 24 hadi 25 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...