Na Wankyo Gati, Arusha

Waziri wa kilimo, Charles Tizeba ameagiza wadau wa pembejeo nchini kuhakikisha wanaweka bei elekezi  ya mbegu katika vifungashio vya mbegu hizo ili kuwawezesha wakulima wasilanguliwe. Hayo ameyasema leo  wakati akifungua mkutano wa wadau wa mbegu uliolenga kupashana taarifa kuhusu maendeleo ya sekta ya mbegu katika kuhakikisha wanazalisha mbegu nyingi na zenye ubora hapa nchini. 

 Waziri Tizeba alisema kuwa , ni lazima vifungashio vyote vya mbegu viwekwe bei elekezi ili kuzuia watu wanaofanya ulanguzi na kusababisha wananchi kushindwa kununua kutokana na bei kubwa wanayotajiwa.

 "naombeni Sana kila kifungashio kitakachokuwa kimebeba mbegu kiwe na bei elekezi na naagiza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya kufuatilia mfumo wa uzalishaji na hizo bei elekezi kwenye vifungashio vyote. "alisema Tizeba.

 Aidha Tizeba pia aliyataka makampuni ya mbegu yanayozalisha mbegu  nje ya nchi na kuuza hapa nchini kuzalisha mbegu hizo hapa hapa nchini ili kuongeza ajira na kuwezesha kulipa kodi na tozo zingine. Alisema kuwa, endapo makampuni hayo yatazalisha mbegu hapa nchini itasaidia mbegu hizo kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu huku kukiongeza upatikanaji wa ajira katika sekta hiyo.

 Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) Patrick Ngwediagi aliwataka wafanyabiashara kupunguza uingizaji wa mbegu toka nje bali wazalishe hapa hapa nchini.

 Aliwataka wafanyabiashara wa mbegu kuhakikisha mbegu zao zinakuwa na lebo ya ubora wa taasisi ya Tosci, kinyume cha hapo mbegu hizo zinakuwa ni feki na hivyo wakulima hawatanunua.

 Kwa upande wa Mkurugenzi wa chama cha wazalisha mbegu Tanzania (TASTA), Bob Shuma alisema kuwa, uagizwaji wa mbegu kutoka nje ya nchi una gharama kubwa Sana kutokana na kodi nyingi zinazotozwa hadi kufika hapa, hivyo endapo uzalishaji huo utafanyika hapa utapunguza gharama hizo huku wakulima wakipewa Kwa bei nafuu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...