Na Veronica Simba – Mara
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali kupitia Wizara anayoisimamia, imejipanga kuhakikisha wawekezaji wote katika sekta ya madini wanatumia umeme katika shughuli zao ili wazalishe kwa tija itakayowawezesha kulipa kodi stahiki kwa Taifa na hivyo kukuza uchumi wa nchi. 

Alitoa kauli hiyo, Septemba 18, 2018 mkoani Mara, wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa Adam Malima ofisini kwake, kabla ya kuanza ziara ya kazi katika Mkoa huo, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

“Tunataka migodi izalishe kwa tija ili kusudi ilipe kodi, ushuru na tozo zote stahiki kwa Serikali hivyo kukuza uchumi wa nchi yetu.”

Kauli hiyo ya Waziri Kalemani, aliitoa kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa kuhusu kuupatia nishati ya umeme Mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo uliopo mkoani humo; ambapo Waziri Kalemani alimhakikishia kuwa Wizara yake inakamilisha taratibu za kuunganisha umeme katika Mgodi huo ndani ya muda mfupi, baada ya mwekezaji huyo kukamilisha malipo.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini, ikiwa ni ishara ya uwashaji rasmi wa nishati hiyo katika eneo hilo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Septemba 18, 2018 kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Kachewa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani humo, kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipowasili katika Mkoa huo kwa ajili ya ziara ya kazi Septemba 18, 2018.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bubombi, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Hafla hiyo ilifanyika Septemba 18, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...