HATIMAYE Canada imeandika historia baada ya kuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kwa kuhalalisha rasmi matumizi ya bangi hadharani kama dawa na starehe. 
 
 
Jarida la Times nchini humo limeeleza kuwa baada ya miaka 95 ya kuzuiliwa kwa matumizi ya bangi hatimaye Canada imetangaza rasmi matumizi ya bangi na soko la kuuza bangi lilifunguliwa rasmi usiku wa kuamkia jumatano. Na hiyo imekuja baada ya watu zaidi ya milioni 15 kutoa maoni yao katika sanduku la posta na kupendekeza uhalalishaji wa matumizi ya bangi. 

Imeelezwa kuwa mwaka 2001 bangi iliruhusiwa kutumika kama dawa na hiyo ni baada ya shinikizo kutoka kwa wabunge nchini humo na kwa sasa watatununua na kutumia bangi hadharani bila bughudhi na polisi watahakikisha na kukabiliana na visa vya uendeshaji magari wakiwa wamelewa bangi. Uhalalishwaji huo umekuja baada ya ahadi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau wa Liberal Party of Canada katika kampeni zake za mwaka 2015. 

Na baadhi ya wananchi wameonekana kununua bidhaa hiyo huku wakipewa risiti ambazo zimekatwa kodi. Historia inaeleza kuwa mwaka 1923 matumizi ya bangi yalipigwa marufuku nchini humo na kufikia mwaka 2001 bangi iliruhusiwa kwa matumizi ya dawa pekee na Oktoba 17 mwaka huu bangi imehalalishwa rasmi kwa matumizi ya dawa na starehe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...