THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DC Uyui Atoa Mkono wa Pole kwa Wananchi Walioathiriwa na Uvamizi wa Tembo

Na Mwandishi wetu- Uyui 

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya amewatembealea na kuwapa pole wananchi walioathirika na uvamizi wa Tembo katika Kijiji cha SawMill Kata ya Migiri. 

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji amesema kuwa ameshawaagiza Askari wanyamapori kufika katika kijiji hicho na kuwaondosha tembo hao ili wasiendele kuleta madhara katika eneo hilo ikiwemo kuharibu mali na kudhuru wananchi . 

“Jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama na wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kama kawaida ndio maana nimewaagiza askari wanyamapori kufika hapa mara moja na kuwaondosha tembo hawa” ; Alisisitiza Msuya 

Akifafanua amesema kuwa tembo hao ambao idadi yao haikufahamika waliingia katika kijiji hicho na kuanza kuharibu mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao katika vihenge. 

Pia aliwataka wananchi katika maeneo hayo kuishi kwa tahadhari kwa kutoa taarifa haraka pale watakapoona wanyama hao wameingia katika makazi yao ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa haraka kuepusha maafa. 

Tembo hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walivamia makazi ya watu usiku wa kumakia tarehe 15 Oktoba na kusababisha uharibifu wa wa mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa wananchi walioathirika na uvamizi wa tembo katika kijiji SawMill Kata ya Migiri Wilayani humo. (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui)