Afanya ziara wilayani Handeni, Lushoto na kuwasha umeme katika Vijiji Vitano

Katika kuhakikisha kuwa adhma ya Serikali ya kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2021 inatekelezwa, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua kazi za usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji.

Akiwa wilayani Handeni, Waziri wa Nishati aliwasha umeme katika Kijiji cha Madebe, Nyasa na Kwamnele na wilayani Lushoto aliwasha umeme katika Kijiji cha Mabugai na Nkelei. Aidha alifanya ziara katika kata na Vijiji mbalimbali ambavyo bado havijasambaziwa umeme ikiwemo Kijiji cha Mahezangulu kilicho katika Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto ambapo aliagiza kuwa, kiwashiwe umeme ifikapo tarehe 12 mwezi huu.

Katika ziara yake wilayani Handeni, Viongozi wa Wilaya hiyo walimweleza kuwa, kuna vijiji 10 ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina nishati hiyo, hivyo kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kuwa walitoa maeneo yao kupisha miundombinu hiyo lakini hawapati umeme. Kuhusu suala hilo, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, kuanzia Jumatatu ya tarehe 8 Oktoba, 2018 wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) waanze utaratibu wa kupeleka umeme katika Vijiji hivyo kwani kinachohitajika ni kusambaza tu umeme kwa wananchi hao kwa kuwa miundombinu ipo.



Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Pili kushoto) akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Madebe wilayani Handeni mkoani Tanga. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe. 


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi kifaa cha UMETA, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Waziri wa Nishati alitoa vifaa vya Umeta 30 kwa Mbunge huyo ili kuwawezesha wananchi kuunganishwa na huduma ya umeme bila kutandaza nyaya ndani ya nyumba.  
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizidua rasmi huduma ya upatikanaji wa umeme katika Kijiji cha Mabugai wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...