Na Lydia Churi-Mahakama Sengerema
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Mahakama itaendeleza ushirikiano uliopo kati yake na mihimili mingine ili kurahisisha suala la utoaji na upatikanaji wa haki nchini.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sengerema ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Jaji Mkuu alisema Mahakama inapata nguvu zaidi ya kutekeleza majukumu yake ya msingi pale inapopata ushirikiano kutoka mihimili mingine yaani Bunge na Serikali.
Alisema endapo Mihimili yote mitatu ya dola haitashirikiana ni wazi kuwa kazi ya utoaji na upatikanaji wa haki itakuwa ni ngumu. Aliongeza kuwa mihimili hii imewekewa utaratibu wa kutekeleza majukumu yake pasipo kuingiliana.
Aidha, Prof. Juma aliipongeza Mahakama ya wilaya ya Sengerema pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema kwa kuwa na uhusiano wa karibu na ushirikiano kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumzia kuhusu rushwa na uvunjifu wa maadili, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania imeamua kupiga vita rushwa na ukosefu wa maadili kwa watumishi wake ambapo pia alimtaka Mkuu wa wilaya ya Sengerema kutosita kuwaita na watumishi wa Mahakama watakaopotoka kwenye suala la rushwa na maadili.
Alisema Mahakama imeamua kutoa nakala za hukumu bure pamoja na kuingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala hizo pamoja na nyaraka nyingine, kama hatua ya kupambana na vitendo vya rushwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bwana Emmanuel Kipole alisema mahusiano kati ya Serikali na Mahakama kwenye wilaya yake ni mazuri kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana bila kuingiliana majukumu.
 Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole akizungumza wakati alipotembelewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini kwake leo.Wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema Mhe. Monica Ndyekobora.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuelezea Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Mhe. Emmanuel Kipole kuhusu kitabu cha Mpango Mkakati wa Mahakama kabla ya kumkabidhi. 
  Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bwn. Samson  Mashalla (wa pili kushoto) akifuatilia jambo wakati wa ziara ya Jaji Mkuu wilayani Sengerema. 
  Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Anatory Kagaruki akielezea jambo kuhusu masuala ya Utumishi wakati Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...