Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mahakimu wameaswa kuzingatia maadili katika utoaji haki ili kulinda heshima yao wenyewe na kuwajengea wananchi imani juu ya mhimili huo.

Hayo ameyasema Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Joachim Tiganga wakati akifungua mafunzo wa mahakimu wanawake katika jiji la Mkoa wa Dar es Salaam yaliyoandaliwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Dar es Salaam.

Tiganga amesema mafunzo yatawajengea uwezo katika utoaji wa haki wa kuepuka mgongano wa kimasilahi.Tiganga amesema ikiwa mahakimu hawatatenda haki katika maamuzi wanayoyafanya watasababisha watu kujichukulia sheria mkononi hali inayoweza kusababisha utovu wa maadili kwa wananchi.

"Nafahamu kuwa Mahakama ya Tanzania iko kwenye kampeni kubwa ya kuhubiri na kusimamia maadili kwa viongozi wa umma na watumishi wake."Mafunzo haya kwetu yamekuja katika muda mwafaka na hii ni ishara kwamba maadili sasa ni wimbo wa kila taasisi ya umma, hasa kwa viongozi wa Umma.Amesema kuwa mafunzo hayo kwa mahakimu wanajibu wa kuzingatia kuzin suala la mogongano wa maslahi kwa sababu ni moja ya mambo yanayosababisha ukiukwaji wa maadili.

Amesema tatizo la mogongano wa kimasilahi limekuwa likizimba nchi nyingi duniani na kusababisha athari katika maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.Aliongeza kuwa mogongano huo wa maslahi hutokea pale ambapo kiongozi mwenye dhamana anapofanya maamuzi na kutumia nafasi yake kutoa haki ndugu, jamaa na marafiki bila kufuata sheria."Unapofanya maamuzi kwa kulinda maslahi ya mtu fulani basi ujue kuwa umejiingiza katika mgongano wa maslahi. Mgongano wa maslahi unasababisha watu wengine kukosa haki na fursa sawa."Jambo hili lisipodhibitiwa linasababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya utoaji haki"amesema Tiganga.

Tiganga amesema kuwa ni vema kiongozi yeyote kujaribu kwa kiasi kikubwa kuepuka mgongano wa kimasilahi na kufanya maamuzi kwa kuzingatia matakwa ya sheria zinazohusika bila upendeleo wala ubaguzi ili kujenga Taifa lenye maendeleo endelevu kwa wote.

Naye Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika kukuza na kusimamia maadili kutokana na utafiti uliofanywa na sekretarieti hiyo kuonesha kuwa ni asilimia moja pekee ya viongozi wanawake ndiyo wanaoshiriki katika utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa maadili."Kwa sababu wanawake ni sehemu kubwa wazazi na walezi, mafunzo haya yatawasaidia kuwalea watoto katika maadili, kwa sababu naamini maadili yanajengwa kuanzia utotoni ndipo tunajenga jamii ya watu wenye maadili," amesema Kipacha.
.Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Joachim Tiganga akuzungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya Mahakimu Wanawake yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalifanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Msajili wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha akitoa maelezo kwa Mahakimu Wanawake katika mafunzo yaliyoandaliwa na Sekretarieti hiyo.
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi Sekretarieti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Katibu Msajili wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha akitoa maelezo kwa Mahakimu Wanawake katika mafunzo yaliyoandaliwa na Sekretarieti hiyo.
picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na Mahakimu Wanawake Katika Mikoa wa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...