Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili wamewasili Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuanzia Oktoba 4 hadi 6, 2018 ikiwa ni ziara ya kikazi kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na vijiji vya Wilaya ya Mbarali.

Makatibu wakuu hao ni kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo; Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Lengo la ziara hiyo ni Kuona na kujiridhisha mambo ambayo yanalalamikiwa kuhusiana na tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN. 28 ya 2008.), kupata suruhu ya kudumu ya uchepushaji wa maji katika mto Ruaha pamoja uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mito na mito.

Maeneo yaliyotembelewa na Makatibu Wakuu hao ni pamoja na eneo chepechepe la Ihefu lililopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mashamba ya mpunga ya madibira (MAMCOS), Banio la maji lililopo eneo la Mnazi kijiji cha Warumba kata ya Ubaruku pamoja na mashamba ya Mpunga ya mnazi katika kijiji cha Mwanavala Kata ya Imalilosongwe.

Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera na Uratibu Prof. Faustin Kamuzora na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Makatibu wakuu wa Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili walipokutana Wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kutembelea maeneo ya shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018.

Baadhi ya Makatibu wakuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) walipohudhuria Kikao kazi hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu walipokutana Wilayani Mbarali ili kutembelea shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018 Mkoani Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...