AWATAKA WAJUMBE WALIOTEULIWA WATHIBITI AJALI NCHINI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wapya wa Baraza hilo ambalo lilizinduliwa hivi karibuni baada ya kuvunjwa na Waziri wa Wizara hiyo mwezi Julai mwaka huu. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akifurahi jambo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa (kushoto) alipokua anazungumza katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo tangu lilipovunjwa Julai mwaka huu kwa lengo la kulifanyia maboresho zaidi. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu alipokua anazungumza kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani katika kikao cha kwanza cha wajumbe wapya walioteuliwa wa Baraza hilo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...