Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MEYA  Mstaafu  wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amempongeza Rais John Magufuli kwa kuruhusu mfumo wa elimu ya bure  katika shule za Msingi na Sekondari na kuwataka wazazi kushirikiana na shule hizo katika maendeleo mbalimbali.

Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya  Shule ya Sekondari ya Mikocheni,Mwenda alisema hatua hiyo ya Rais Magufuli imesaidia wanafunzi pamoja na wazazi wengi kunufahika na elimu hiyo.

Alisema ukilinganisha na miaka ya nyuma,hivi sasa wanafunzi wengi  wanapata elimu tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo wengi waliikosa kutokana na kushindwa kulipia ada za shule.Mwenda alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake tangu aingie madarakani, amejenga shule nyingi katika kata mbalimbali, jambo lililowawezesha wanafunzi wengi na jamii kunufahika.

"Kinachotakiwa kwa sasa ni wazazi kutoa ushirikiano kwa shule hizo ili ziweze kupata nguvu ya kusonga mbele kimaendeleo na kuinua kiwango cha elimu nchini alisema Mwenda.Aliwataka wazazi pia kutambua kuwa licha ya Serikali kutoa elimu  bure, bado wanapata kuchangia maendeleo ya shule hizo hatua itakayozisaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Aidha aliwapongeza wahitimu katika mahafali hayo na kuwataka kuwa mfano kwa kufanya vizuri katika mtihani wao mwisho na hivyo kufungua njia yao ya kimaisha lakini pia kuwapa hamasa wanafunzi waliobakia shuleni hapo. Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Salama Ndyetabura alisema shule hiyo iliyoanzishwa miaka minne iliyopita pamoja na mafanikio baadhi iliyoyafikia,bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa maabara.

Alisema pamoja na changamoto hiyo,pia shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madras pamoja na walimu wa masomo ya sayansi suala aliliiomba Serikali kulitatua.Jumla ya wanafunzi 158 walihitimu katika mahafali hayo wakiwemo wavulana 79 na wasichana 79.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...