Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
MFANYABIASHARA na mmiliki wa mabasi ya Princes Muro, Majid Abdallah maarufu kama Kimaro (51) leo Oktoba 23.2018  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la wizi na utakatishaji wa mafuta.

Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali, Esther Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa mshtakiwa ametenda makosa hayo kati ya Januari 2015 na Januari 2018 katika maeneo tofauti ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la wizi imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa aliiba Lita 15950.3 za Mafuta aina ya Diesel na Lita 10925.22 za Mafuta aina ya Petrol mali ya mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Katika shtaka la utakatishaji, imedaiwa, siku hiyo katika sehemu tofauti tofauti za jiji la Dar es Salaam,mshtakiwa alitakatisha Lita hizo za Mafuta  kwa kuyauza  na kuyabadilisha kwa fedha huku akijua kuwa mafuta hayo ni zao la kosa la wizi naa alifanya hivyo kwa lengo la kupoteza uhalisia wa mafuta.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo Kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikilizwa kesi za uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 5, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Princes Muro, Majid Abdallah maarufu kama Kimaro (51) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili pamoja na shtaka la wizi na utakatishaji wa mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...