*Waziri Mkuu aagizwa achukuliwe hatua
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi
awachukulie hatua askari polisi wote wa wilaya ya Kyerwa wanaotuhumiwa
kusindikiza kahawa ya magendo inayouzwa nchi jirani akiwemo Mkuu wa
Polisi wa Wilaya hiyo, Justin Joseph.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 7, 2018) baada ya kukagua kiwanda cha
kukoboa kahawa cha Nkwenda wilaya Kyerwa katika siku ya pili ya ziara
yake ya kikazi mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana
na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
“Askari
polisi wa wilaya ya Kyerwa pamoja na OCD wao wanatuhumiwa kusindikiza
kahawa inayosafirishwa kwa njia ya magendo kwenda nchi ya jirani kupitia
njia mbalimbali zisizo rasmi zikiwemo za Kumisongo, Kashaijo na
Omukatoma.”
Waziri
Mkuu amesema ni jambo la hatari kama askari Polisi wanasindikiza kahawa
inayouzwa kwa magendo, hivyo ameagiza jambo hilo lidhibitiwe
haraka.”Marufuku kupeleka kahawa nje ya nchi kwa njia ya magendo na
polisi msishiriki katika butura.”
Katika hatua nyingine,Waziri
Mkuu amesema kuanzia msimu ujao wa kahawa, minada yote ya kahawa
inayozalishwa mkoani Kagera itafanyika ndani ya mkoa huo badala ya
kufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Kaderes
kilichopo eneo la Nyakatuntu wilayani Karagwe Oktoba 7, 2018. Kulia ni
Mkewe Mary na kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda, Leonard Kachobonaho.
Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha
Gaguti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakimfariji mtoto ,
Mathews Martin aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Kayanga wilayani
Karagwe, Oktoba 7, 2018. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Joyce Martin.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya
kutembelea Kituo cha Afya cha Kayanga kilichopo Karagwe, Oktoba 7, 2018.
Wapili kulia ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati
walipowasili kwenye uwanja wa Kayanga Changarawe, Karagwe kuhukutubia
mkutano wa hadhara, Oktoba 7, 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...