THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

PROF. MDOE: WANAFUNZI 124,000 KUNUFAIKA NA MKOPO WA ELIMU YA JUU

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAOFISA wanaosimamia madawati ya mikopo vyuoni wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora isiyokuwa na urasimu na badala yake wahakikishe wanaimarisha madawati hayo ili kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na uhitaji wanufaika na mikopo kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati akizungumza katika kikao kazi cha siku mbili cha maafisa hao kilichoanza mjini Bagamoyo.

Amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata Elimu ya juu bila kikwazo.

Profesa Mdoe amesema kwa mwaka wa fedha 2018/19 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 427. 5 ambapo jumla ya wanafunzi 124 watanufaika na mkopo huo, na kuwa ugawaji wa mikopo hiyo uzingatie haki, vigezo, kanuni na sheria.

“Nataka twende vizuri tukahakikishe huduma bora inatolewa katika mwaka huu mpya wa masomo ikiwa ni pamoja kutoa huduma bora,kusimamamia kumbukumbuku na kuhakikisha mawasiliano ya mara kwa mara yanakuwepo kati ya maafisa mikopo na bodi ya mikopo na kwa haipendezi maafisa mikopo kuwa chanzo cha migogoro,”amesisitiza Profesa Mdoe.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB )Abdul- Razq Badru akitoa taarifa ya bodi hiyo katika mkutano wo katika bodi na maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu nchini katika mkutano uliofanyika mjini Bagamoyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu uliofanyika mjini Bagamoyo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq Badru.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adam Mwakalobo akizungumza kuhusiana na ofisi yake inavyoratibu masuala ya elimu ya juu nchini kwa kushirikiana na vyuo vikuu,katika mkutano wa maafisa wa mikopo vyuo vikuu ulifanyika mjini Bagamoyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa mikopo wa vyuo vikuu.