Raia wa Sudan Nada Zaelnoon Ahmed Elbokhary(38) aliyejifunika kitambaa chekundu akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa shtaka moja la kukutwa na fedha za Dubai kiasi cha zaidi ya milioni 120 ambazo ameshindwa kuzitolea taarifa ya fedha.

Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii
RAIA wa Sudan, Nada Zaelnoon Ahmed Elbokhary(38), anayeishi Masaki jijini Dar es salaam, Leo Oktoba 15/2018 amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kukutwa na fedha za Dubai kiasi cha zaidi ya milioni 120 ambazo ameshindwa kuzitolea taarifa ya fedha.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Oktoba 9, 2018 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini.
Imedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa Elbokhary wakati akiondoka katika nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Sudan, alikutwa akiwa na USD 60,000 ambazo ni zaidi ya sh. milioni 120 na Sudanese pound 3410 ambazo hakuzitolewa maelezo kwa mamlaka wa forodha.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh.milioni 20.

Pia mahakama imemtaka  kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo

 Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 22 Mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH) kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...