Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya Follow the Honey Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa asali nchini ili kuchagiza uzalishaji wa asali nchini na kukidhi soko la kimataifa.

Nia hiyo imewekwa wazi wakati wa kikao cha pamoja kati ya uongozi wa kampuni hiyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa Benki ya Kilimo ipo tayri kushirikiana na wadau mbalimbali wenye lengo la kuwawezesha wafugaji wadogo wadogo wa nyuki ili waweze kufuga kisasa nyuki ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji wa asali ili waweze kufikia mahitaji ya soko.

Bw. Justine aliongeza kuwa TADB inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya uongezaji wa thamani wa ufugaji wa nyuki

“Lengo la benki ni kuwaongezea uwezo wafugaji wadogo wadogo wa nyuki ili waweze kujiongeza kipato,” aliongeza.

Kwa upande Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bw. Kaizirege Camara alisema kuwa kampuni yake imejipanga kusaidia wafugaji wa asali nchini kufikia soko la kimataifa kwa kuwasaidia kuzalisha kisasa asali zao.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (wapili kulia) akizungumza na ugeni kutoka na Kampuni ya Follow the Honey Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa asali nchini kuhusu utayari wa TADB katika kuchagiza uzalishaji wa asali kwa ajili ya kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Wanaomsikiliza ni Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa kampuni hiyo, Bibi Mary Canning (kushoto) na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Kaizirege Camara  (wapili kushoto). Wengine ni Meneja wa Biashara wa TADB, Bw. Dickson Pangamawe (kulia) na Afisa Masoko wa Follow the Honey Tanzania, Bi. Sarah Kibambaza (katikati).
 Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bibi Mary Canning (kushoto) akieleza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (kulia). Bibi Canning aliongozana na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania,  Bw. Kaizirege Camara  (wapili kushoto) na Afisa Masoko wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bi. Sarah Kibambaza (wapili kulia).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (katikati) akifurahi jambo na Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bibi Mary Canning (kulia) wakati wa maongezi yao.
Uongozi wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (katikati) mara baada ya mazungumzo yao kuhusu uzalishaji wa asali nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...