Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Serikali
imepiga marufuku kwa madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa majina ya
kibiashara badala yake watumie majina ya asili (Generic name). Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa
Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania
Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar
es Salaam.
Dkt.
Ndugulile amesema imefika wakati serikali imebidi kutoa tamko hilo
kwasababu Madaktari wengi wamekuwa wakikiuka miongozo wa utoaji matibabu
uliotolewa na wizara ya afya. "Katika mfumo wa utoaji wa huduma za
afya, tunamtaka daktari aandike kwa jina la asili ili mfamasia
akatafsiri aina ile ya dawa tulizonazo kwenye akiba yetu za dawa
tulizonazo, ubora wa dawa za Tanzania ni za kiwango cha juu kabisa,
tuwaambie wa Tanzania waache zile dhana potofu akisikia zile
zinazotoka," amesema.
Amesema
kinachotokea kwasasa katika hospitali nyingi unakuta madawa ni mengi
ila hayatumiki wanaishia kwenda kununua nje wakati angeandika kwa jina
halisi angepatiwa. Amewataka wafamasia na waganga wafawidhi wa hospitali
zote nchini kuhakikisha wanatoa orodha ya dawa zote walizonazo kila
mwanzo wa wiki ili kuwawezesha watoa dawa kufahamu dawa walizonazo ili
kuondoa adha kwa wananchi kuandikiwa dawa ambazo hazipo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai akizungumza machache wakati akitoa neno la utangulizi katika Ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa -Tanzania linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula akitoa shukrani zake za pekee kwa waandaaji wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai.
Washiriki wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...