NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

SEKTA ya elimu mkoani Pwani, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 3,678 katika shule za msingi pamoja na nyumba za walimu 5,188.


Kufuatia changamoto hiyo ,kampuni ya Sayona fruits ,iliyopo Mboga huko Chalinze imetoa mabati 1,000 yenye thamani ya sh.mil 24 ,kwa ajili ya umaliziaji wa majengo mbalimbali ya shule za msingi mkoani humo .

Akipokea mabati hayo ,kutoka kwa mkuu wa kitengo cha mahusiano cha kampuni hiyo ,Abubakar Mlawa , mkuu wa mkoa wa mkoa huo mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,wanakabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na halmashauri,jamii na wadau wa elimu . “Miundombinu ya shule za sekondari na hasa shule za msingi bado kuna upungufu ,ambapo mkoa una jumla ya shule za msingi 613 huku za serikali zikiwa ni 562 na 51 ni za watu binafsi “

“Shule za msingi pekee mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 700,671, yaliyopo 3,993 na upungufu ni vyumba vya madarasa 3,678 ” alifafanua Ndikilo. Ndikilo alitaja pia tatizo la nyumba za walimu ili waweze kuishi vizuri hivyo kuna mahitaji ya nyumba hizo 6,779 . Alisema ,nyumba zilizopo ni 1,591 na upungufu ni nyumba za walimu 5,188.

Akipokea msaada wa mabati , mkuu wa mkoa wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto )kutoka kwa mkuu wa kitengo cha mahusiano cha kampuni ya Sayona fruits iliyopo Mboga Chalinze ,Abubakar Mlawa (kulia) ,msaada ambayo umeelekezwa kuimarisha sekta ya elimu .( picha na Mwamvua Mwinyi ).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...