MKUU wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ametoa wasilisho la chaneli za maudhui ya bila kulipia kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Akizungumza mbele ya madiwani hao leo Mhandisi Mihayo amewaambia madiwani hao mkakati wa TCRA ni kuhakikisha wenye visambusi wanafuata leseni zao ili kutoa fursa kwa Watanzania kupata haki ya kuona chaneli kama ambavyo leseni zinavyoelekeza. Hivyo amewataka madiwani hao kuwaeleza wananchi kuhusu visambusi ambavyo wanatakiwa kununua na ili kuona chaneli zote muhimu bila kulipia. 

 "Madiwani wetu tunawaomba muwaambie wananchi wanunue visambusi vya TING, DigTeck,Startimes na Contineto ambavyo ndivyo vyenye leseni ambazo zinawapa uhalali wa kuonesha chaneli za nyumbani,"amesema Mhandisi Mihayo. Amefafanua baada ya kuona kuna wamiliki wa visambusi wanakiuka taratibu ilifunguliwa kesi mahakamani na baada ya kushinda wakaona ni vema watu wakaumia alau kidogo lakini kurudisha utararibu ambao upo kisheria katika kuonesha chaneli za nyumbani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...