BENKI ya TPB, imetoa msaada wa fimbo nyeupe 20 kwa chama cha wasioona tawi la Dar es Salaam, zenye thamani ya sh milioni 1. Msaada huo ulitolewa jana na Meneja wa Mawasiano wa Benki ya TPB, Bi. Chichi Banda na kukabidhiwa Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Seif Jega. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bi Chichi Banda alisema benki hiyo ilitoa msaada huo kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika jamii. ‘’Katika uendeshaji wa benki yetu, huwa tuna utaratibu wa kutenga kiasi cha faida kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii katika maeneo makuu matatu ambayo ni afya, elimu na ustawi wa jamii’’. Hivyo basi tunawaomba wananchi muendelee kutuunga mkono kwa kutumia huduma zetu za kibenki kwani tunachokipata kama faida, mara zote tumekuwa tukirudisha kwenu kupitia misaada tunayotoa’’, alisema Chichi. ‘’Tunaamini msaada huu, utaenda kupunguza changamoto kwa wale wasioona ambao walikosa kifaa hiki muhimu katika maisha yao’’, aliongeza Chichi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Seif Jega, aliushukuru uongozi wa benki ya TPB kwa msaada huo ambao utawasaidia katika maadhimisho ya SIKU YA FIMBO CHEUPE dunia utakaofanyika kitaifa mkoani Mwanza siku ya tarehe 25 Oktoba 2018. Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Makamu wa Raisi, Mhe. Mama Samia Suluhu. ‘’Kwa kweli tumefarijika sana, kupokea huu msaada kutoka benki ya TPB, na tunaahidi tutaufikisha kwa wanachama wale ambao walikuwa hawajapata bado fimbo hizi’’, alisema Jega. 
Cheo: Meneja Mawasiliano
Jina: Chichi Banda
Namba: 0682 136414
Meneja Uhusiano wa Benki ya TPB, Bi. Chichi Banda (kulia) akikabidhi fimbo cheupe 20 zenye thamani ya sh milioni 1 kwa chama wa wasioona mkoa wa dar es salaam. Akipokea msaada huo ni Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Seif Jega (katikati) aliyeambatana na Mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho Bi Lucy Bupamba (kushoto). Fimbo hizo zitatumika katika maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe duniani, ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Mwanza oktoba 25. 
Meneja Uhusiano wa Benki ya TPB, Bi. Chichi Banda (kulia) akikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh milioni 3.9 kwa Jeshi la Magereza Tanzania. Akipokea msaada huo ni Mrakibu Msadizi wa Magereza (Afisa Michezo Jeshi la Magereza) ASP Bakari Sudi (katikati), akishuhudia tukio hilo ni SGT Edwin Masinga ambaye ni kocha mkuu wa timu ya mpira wa volleyball Magereza. Vifaa hivyo vitatumika siku ya Michezo ya Wanajeshi Tanzania (BAMMATA) itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi Novemba. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nashukurukutuhabarisha
    Naona umeswap ya magereza ngu za michezo
    na wanaopokea fimbo nyeupe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...