Na Mwandishi Wetu, Mihambwe 

Mara nyingi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza maendeleo hayana chama akiwa na maana kwenye suala la maendeleo tuweke pembeni itikadi za kisiasa na tuungane kuleta maendeleo. 

Kauli inayofanana na hiyo imesemwa na Afisa Tarafa wa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu wakati alipotembelea mradi wa maji wa kijiji cha Mihambwe uliopo kata ya Mihambwe ambapo ameshangazwa na mradi mzuri wa maji kutokufanya kazi kutokana na misuguano ya kisiasa. 

“Hii tabia ya kupangua pangua maamuzi halali ya vikao, tabia ya mivutano ya kisiasa isiyo na tija ni sehemu ya tatizo ya kusimama kwa mradi huu. Ulivyo simama mmepata faida gani? Wewe uliyesababisha hauathiriki na tatizo la ukosefu wa maji? Acheni hizi tabia, tushirikiane kwa pamoja tuhakikishe mradi huu wa maji ufanye kazi tena kama awali” alisema Gavana Shilatu wakati alipotembelea eneo lilipo mradi huo wa maji. 

Wakizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji alimwomba Gavana Shilatu azidi kuwaunganisha zaidi wawe kitu kimoja. 

“Leo hili kwetu ni tukio la kipekee la sote kwa pamoja kukutana na kujadili mambo ya kimaendeleo. Ninamwomba Afisa azidi kuitisha vikao vya kutuunganisha na kutuweka kwenye mstari mmoja. Kiukweli nimependa sana anavyotuleta pamoja kwenye masuala ya kimaendeleo.” alisema Mjumbe wa Serikali ya Kijiji ya Mihambwe. 

Ziara hiyo ya kutembelea mradi wa Maji, Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata, Afisa Maendeleo kata ya Mihambwe, Serikali ya Kijiji cha Mihambwe pamoja na Wajumbe wa kamati ya mradi wa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...