Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa mifugo na uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika suala la ufugaji wa kuku.Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja  na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao.

Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa ili kuweza kuendeleza shughuli za hizo.Kuhusiana na changamoto zilizotolewa na wafugaji hao hasa katika mashudu na soya ambazo huagizwa kutoka nje Ulega amesema kuwa maandalizi yameanza katika nyanda za juu kusini ambako soya zimelimwa na wanavutia uwekezaji katika usindikaji ili kuweza kuvutia uwekezaji wa kuchakata soya na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.

Kuhusiana na machinjio zinazochinja kuku Ulega amesema kuwa sehemu hizo zimekuwa na ubora wa chini sana na amewataka wahakikishe wanaboresha machinjio hayo yanayosimamiwa na halmashauri na manispaa hasa kwa kuzingatia wanaweka  sehemu ya machinjio ya kuku ili kuleta thamani.Mwenyekiti wa chama cha ndege wafugwao Harko Bhaghat amemshukuru Naibu waziri na wizara kwa ujumla kwa kutoa kipaumbele kwa wafugaji na kusema kuwa hadi sasa wamepata mafanikio makubwa na kubwa zaidi ni baada ya serikali kuondoa tozo katika bidhaa za mifugo.

Bhaghati amewataka wafugaji kujisajili ili waweze kupata fursa mbalimbali za kuendeleza soko la ndege wafugwao hasa kuku.
Naibu Waziri wa  Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa ndege wafugwao, katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya ndege wafugwao nchini jana jijini Dar es Salaam . (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya Jamii)
 Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa ndege Harko Bhaghati akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega.
 Mtaalamu na mshauri wa mifugo kutoka kampuni ya Animal Care Dkt. Bakari Mwanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  kuhusu uzalishaji na utunzaji wa mifugo unaofanywa na kampuni yao.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wafugaji waliojitokeza ili kupata semina na mafunzo kuhusiana na ufugaji wa kuku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...