Na Mwandishi Wetu, Tanga
SERIKALI ya Tanzania ikishirikiana na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa wamefanya tamasha kubwa la vijana mjini Tanga, mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana nchini Tanzania.
Tamasha hilo ambalo lilishirikisha vijana 500 limewezeshwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa ya UNESCO, UN Women na UNFPA kwa kushirikiana na Serikali.
Katika tukio hilo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume. Tamasha hilo liliwakumbusha vijana ushiriki wao katika malengo ya dunia kupitia michezo ukiwamo soka.
Wakiwa na wito wa nafasi salama ya vijana, michezo imetumika katika kushawishi vijana kujieleza na kuimarisha uwezo wao wa kimichezo ili kuchangia utekelezaji wa malendo endelevu ya dunia.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2013 lilipitisha Aprili 6 kuwa siku ya michezo kwa maendeleo na amani.
Siku hiyo huadhimishwa kwa kuwaleta pamoja watu wengi katika michezo kama sehemu ya kuwa na amani, kutengeneza uvumilivu na heshima.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, amewataka vijana kutambua wajibu wao na kutekeleza mipango endelevu ya nchi huku wakijihakikishia usalama wao.
Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo kwenye bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Aidha alirejea ujumbe wa Mwenge mwaka huu ambao umesisitiza mapambano ya Ukimwi, Malaria na matumizi ya dawa za kulevya na mapambano dhidi ya ufisadi kwa Tanzania.
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba katika bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigella.
 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Sehemu ya vijana kutoka shule mbalimbali pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Baadhi ya wanafunzi wakipozi na mabango ya malengo ya maendeleo endelevu wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...