Na Bashir Yakub.

Ardhi iwe kiwanja au nyumba thamani yake hupanda pale inapokuwa imepimwa. Kupima ardhi ni kurasimisha ardhi. Faida nyingi hupatikana baada ya ardhi kuwa imerasimishwa. Baadhi ya faida ni kuwa ardhi hupanda thamani yake, kuweza kupata mkopo kwa urahisi, ardhi kutumika kama dhamana mahakamani, lakini kubwa ni kuwa na amani na uhakika wa ardhi yako kuwa eneo ulilopo linaruhusiwa kisheria, sio eneo hatarishi, sio eneo la miradi ya serikali, sio hifadhi ya barabara au barabara nk. Unakuwa na amani kuwa uko sehemu sahihi na salama. 

Kupima ardhi ni hatua inayopitiwa pale unapoelekea kupata hati. Kila ardhi yenye hati imepimwa lakini si kila ardhi iliyopimwa ina hati. 

UTRATIBU WA KUPIMIWA ARDHI. 

1.Kuandika barua ya maombi ni hatua ya kwanza ambapo utatakiwa kumwandikia mkurugenzi wa halmashauri ukiomba kupimiwa eneo lako. Hii ni barua ya kawaida ya kiofisi isipokuwa ieleze majina yako kwa ukamilifu na ichambue anuani ya eneo ambalo linalotakiwa kupimwa kwa ukamilifu.Mkurugenzi unayetakiwa kumwandikia ni yule wa halmashauri ambamo ardhi inayotakiwa kupimwa imo. Kwa mfano kama ardhi iko wilaya ya kinondoni basi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya atakayeandikiwa barua. 

Barua hiyo itaambatanishwa na nyaraka za umiliki wa eneo husika. Mara nyingi nyaraka hapa huwa ni ile mikataba ya mauziano. Kadhalika, barua yako inatakiwa kupitishwa serikali za mitaa na kwa mtendaji kata.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...