Wakulima, katika skimu ndogo ya kilimo cha mbogamboga ya Iganjo Iliyopo Iliyopo Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya, wameomba wataalam kutoka wakala wa vipimo kuwatembelea ili kuweza kusaidia tatizo la vipimo halisi vya mazao yao ambavyo vinafanywa katika hali ya udanganyifu na kuwasababishia hasara. 

Hayo yemeelezwa na Mwenyekiti wa chama cha Wamwagiliaji Iganjo Bw. John Soda alipokuwa akizungumza katika eneo hilo mbapo alisema kuwa suala la kuzidisha ujazo unaotakiwa (lumbesa) bado ni tatizo jambo ambalo linawasababishia wao kama wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya hasara.

Bwana Soda alisema kuwa kumekuwa na tatizo la upimaji wa mazao katika magunia ambapo magunia yanayokaguliwa yanakuwa na vipimo halisi lakini magunia yanayokwenda sokoni yanakuwa hayana uhalisia. Tunawaomba wakala wa vipimo waweze kuja kututembelea na kusimamia kwa ukaribu swala hili la udanganyifu katika vipimo, jambo ambalo kwa kiasi fulani limekuwa likitusababishia hasara sisi wakulima wa mboga mboga hasa katika zao la viazi, vitunguu na karoti, Pamoja na hilo naiomba serikali iweke utaratibu wa kuuza mazao na kutoa bei elekezi.” Alisema Bwana Soda.

Kwa Upande wake Bwana Solomon Soda Mkulima katika skimu hiyo aliishukuru Serikali kwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika skimu hiyo na kuiomba iendelee kuwasaidia waweze kupata pembejeo kwa bei ya ruzuku, na kumalizia kuboresha miundombinu katika sehemu iliyobakia.

Katika picha ni Miundombinu mfereji wa maji unaopeleka maji katika skimu ya umwagiliaji Iganjo Uyole mkoani Mbeya, pembeni yake ni shamba la mahindi yanayomwagiliwa kwa kutumia maji yanayopita katika mfereji huo. 

Bwana John Soda mkulima katika skimu ya Iganjo Uyole Mkoani Mbeya akizungumza kuhusu ukarabati uliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika skimu hiyo, inayoonekana kwa nyuma ni sehemu ya miundombinu hiyo.

Katika Picha ni banio linaloruhusu maji toka chanzo cha maji cha mto Nkwanana kupeleka katika skimu ya umwagiliaji ya iganjo iliyopo Uyole mkoani Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...