Na Mwandishi wetu, Kondoa

WAKULIMA wa Mbaazi na Choroko hapa nchini wanatarajia kuondokana na adha ya mazao yao kukosa soko baada ya wawekezaji kadhaa kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao hayo katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro.

Kauli hiyo ya matumaini kwa wakulima hao imetolewa wilayani Kondoa mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, wakati akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

" Kilimo kinategemewa na zaidi ya asilimia 65 ya watanzania, lakini zao la mbaazi limekuwa na matatizo ya soko ndio maana Serikali imeamua kuchukua hatua kwa kuwahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika mazao hayo hapa hapa nchini, jambo ambalo limeanza kutekelezwa" alisema Mhe. Mgumba

Alisema hivi sasa viwanda vitatu vya  kuchakata mbaazi vinajengwa mkoani Arusha, Dar es Salaam na Morogoro katika eneo la Mtego wa Simba, huku kiwanda kimoja na kusindika choroko kikijengwa mkoani Dodoma.

Alisema kuwa lengo la hatua hizo ni kujibu kero ya muda mrefu ya wakulima wa mazao hayo katika mikoa ya Manyara, Arusha, Dodoma na maeneo mengine yanayolimwa mazao hayo  kukosa soko la uhakika kwa kuongeza thamani ya mazao hayo hapa hapa nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katika Jimbo la Kondoa, uliofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...