Na Zuena Msuya,  Singida
SERIKALI imeanza kulipa fidia kwa wananchi 4000 waliopisha mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400  kutoka Singida hadi Namanga ambapo zoezi la ulipaji fidia litakamilika hivi karibuni.
Mradi huo wa kusafirisha umeme wa kV400 kutoka Singida hadi Namanga utaunganisha nchi za Tanzania na Kenya na unafahamika kama  (Kenya – Tanzania Power Interconnector Project), (KTPIP).

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu alisema hayo alipotembelea eneo la kuhifadhia vifaa vya mradi huo (yard)  katika kijiji cha Nangwa wilayani Hanang mkoani Manyara, mwishoni mwa wiki, ili kukagua vifaa hivyo vitakavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya umeme.

Mgalu alisema kuwa, kazi za awali za utekelezaji wa mradi huo zilikwishaanza na kinachosubiriwa sasa ni kukamisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi husika ili wakandarasi waanze rasmi kazi ya ujenzi.

Mgalu aliweka wazi kuwa, katika utekelezaji wa mradi huo, vijiji 14 vilivyopitiwa na mradi vitapata umeme ambapo vijiji 7 ni vya  Mkoa wa Singida, 2 kutoka Mkoa wa Manyara na 5 ni vya Mkoa wa Arusha.
 Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akikagua yadi ya kuhifadhia miundombinu ya kujenga mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa 400kv kutoka Singida hadi Namanga.
 Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu( kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa  wa 400kV, Mhandisi Oscar Kanyama,( kulia) wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo alipotembelea yadi hiyo kukagua vifaa na miundombinu ya kutekeleza mradi huo. 
Baadhi ya vifaa vilivyohifadhiwa katika yadi ya kuhifadhia vifaa na miundombinu ya kujenga mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa 400kV kutoka Singida hadi Namanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...