Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na kuingia Serengeti.

Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na wageni kulipa jina la “Great Wildebeest Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea kushuhudia tukio hilo.Michuzi blog imeshuhudia Msururu wa Magari ya kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa makundi kutoka upande mmoja wa mo kuingia Hifadhi ya Serengeti.

Eneo la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10 hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa sababu si rahisi kufahamu wapi wataelekea kuvuka jambo ambalo hutumia zaidi ya saa 5 hadi 7 kungojea tukio hilo.Tukio la misafara ya makundi ya wanyama hao kuhama na kurudi hubadilika kila mwaka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kiwango cha maji katika mto mara hata hivyo limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni .

Kivutio kikubwa katika misafara ya wanyama hao ambao wamekuwa wakiondoka nchini kila mwaka kuanzia mwezi mey na kurudi kuanzia mwezi julay ni namna wanavyovuka mto mara na jinsi wanavyokabiliana na wanyama wengine ndani ya mto huo wakiwemo Mamba.

Watalii wakiwa kando ya Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,eneo la Kogatende wakishuhudia tukio kubwa la kuhama kwa Makundi Makubwa ya Nyumbu wakivuka mto kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kundi la Nyumbu likijiandaa kuvuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Nyumbu wakivuka Mto Mara kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .

Magari yaliyobeba Watalii yakiwa yameegeshwa kando ya Mto Mara kusubiri tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu katika Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mamba wakiwa Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa katika mawindo ya Mnyama Nyumbu wakati akivuka.

Mnyama Pundamlia wakiwa upande wa pili mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,tunaweza sema ni kama wako hapo kwa ajili ya mapokezi ya Nyumbu wanarudi kutoka katika Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...