Na WAMJW-DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
imewaasa Watanzania kujijengea tabia ya kupima macho mara kwa mara ili
kuweza kuepuka aina mbalimbali za magonjwa ya macho ikiwemo vikope.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga
Mkuu wa Serikali Dkt. Eliud Eliakimu wakati wa kufungua hafla ya
kuelekea siku ya Afya ya Macho Duniani ambayo huadhimishwa kila alhamisi
ya Pili ya mwezi Octoba.“Asilimia kubwa ya magonjwa ya
macho yanatibika ikiwemo upeo mdogo wa macho kuona ambao yanazuilika
kwa miwani endapo mtu akiwahi katika kituo cha kutolea huduma za Afya
na akigundulika ana tatizo la macho basi atapata matibabu mapema”alisema
Dkt. Eliakimu.
Aidha, Dkt. Eliakimu alisema kuwa
kwa Tanzania watu wasioona kabisa ni asilimia moja sawa na watu laki 5.7
huku watu wenye matatizo mbalimbali ya macho wanakadiriwa kuwa mara
tatu ya wasioona kabisa sawasawa na mil.7.Kwa mujibu wa Dkt. Eliudi amesema
kuwa takwimu zinaonesha kwamba ugonjwa wa macho umepungua kutoka
asilimia 4.6 mwaka 1990 na kufikia asilimia 3.4 mwaka 2015 kutokana na
hamasa ya juu ya upimaji toka kwa wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja
Mpango wa Huduma za Macho Nchini kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Benadertha Chilio amesema kuwa
tatizo la macho linaloongoza nchini ni mtoto wa jicho ambapo wagonjwa
wanafikia kwa asilimia 50 na wengi wao ni wanawake.
Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt. Eliud Eliakim (Kushoto) akimkabidhi Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa huduma za macho Dkt. Bernadetha Chilio kitabu cha muongozo wa utoaji huduma za macho katika maadhimisho ya wiki ya afya ya macho yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.
Washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakiwa katika maandamano kuadhimisha wiki ya afya ya macho yaliyofanyika jijini Dodoma mapema leo.
Kaimu Mganga Mkuu Wa Serikali Dkt. Eliud Eliakim akipata maelezo kutoka Titus Nyange jinsi mashine ya Perkins inavyochapa nukta nundu zinazosomwa na watu wenye ulemavu wa macho wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya ya macho duniani yanayofanyika jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...